Friday, October 19, 2007

AGIZO LA KUACHA KUPAKIA ABIRIA ZAIDI LAPUUZWA

Agizo la kuacha kupakia abiria zaidi katika mabasi lapuuzwa 2007-07-18 20:09:17 Na ITV Habari



Agizo la waziri mkuu la kutaka mabasi ya abiria kutozidisha abiria ili kuepusha ajali bado linapuuzwa na baadhi ya wasafirishaji wilayani Kondoa. Baadhi ya mabasi ya kampuni moja ya usafirishaji yameonekana kuwa ndiyo yanayoendekeza tabia hiyo kwa kile baadhi ya abiria walichoeleza kuwa ni kuogopwa na askari wa usalama barabarani. ITV imeshuhudia mkuu wa wilaya hiyo kepteni Seif Mpembenwe akizuia basi moja lililokuwa limesheheni abira hadi katika sehemu ya mizigo, huku wengine wakining`inia.
SOURCE: ITV

No comments: